Adele atufunze kuheshimu na kukubali uwezo wa wengine

Adele atufunze kuheshimu na kukubali uwezo wa wengine

Like
340
0
Monday, 20 February 2017
habari

Kukubali kile ambacho mwingine anacho ni moja kati ya ishara na namna fulani ambayo inaonyesha kua mwanadamu amekomaa kifikra na kiakili kuwa pamoja kuwa anajikubali juu ya uwezo wake lakini anaweza kumpa mwingine heshima yake inapostahiki kufanya hivyo.

Siku kadhaa zilizopita mwanamuziki Adele alishinda tuzo za Grammy na moja kati ya tunzo alizoshinda ni katika kipengele cha album bora akimshinda Beyonce aliyekuwa akiwania tunzo hiyo pia. Cha kusisimua ni pale Adele alipokiri hadharani kua hakudhani Kama alistahili tuzo ile mbele ya Beyonce!

Kukubali hayo achilia mbali kukiri hadharani inahitaji akili iliyokomaa na yenye kujiamini haswa. Kuwa pamoja na kwamba unaamini una uwezo na kipaji lakini haikufanyi usione ubora wa mwenzio katika jambo fulani. Lile tukio halikuondoka na chochote kwa Adele zaidi ya kumuongezea thamani mbele ya Beyonce na jamii ya muziki duniani kote kwa ujumla.

Natamani kuona wasanii wa nyumbani wa kijifunza katika hili,kukubali uwezo na kipawa cha mwingine. Ni jambo nadra kukuta tukio la Nay wa mitego kukiri hadharani kuwa hadhani kama ni sawa kwa rapa mwepesi kama yeye kulinganishwa na mtu Kama Fid Q. Huwa inatokea mara chache sana. Lakini ilichukua chochote kutoka kwa Nay wa Mitego? No alijiongezea heshima tu.

Sio lazima wote twende hadharani na kukiri uwezo wa wasanii au wanamuziki wenzetu hata kwenye mioyo yetu na fikra zetu tukaona na kutambua lile wenzetu walilonalo ama walilopigana kua nalo itakuwa ni hatua kubwa katika kujua nini ufanye ili uweze kufika pale mwenzio alipofika pengine hata zaidi yake.

Ni wazi hatuwezi kupiga hatua kama mioyo na fikra zetu zitaishi zikiamini watu fulani kwenye game wamefanikiwa au wanafanikiwa kwa sababu ya fitna na michezo michafu na wala sio vipaji na juhudi wanazoziweka katika kufanikiwa. Kukubali na kuheshimu vilivyomo kwa wenzetu ni kujiamini kuwa wewe unaweza.

Kujifunza ni hatua inayoanzia kwenye kugundua nini huna, ili ugundue kile ambacho wewe huna lazima uangalie kwa waliofanikiwa hata kama ni washindani wako kiasi gani. Kukubali na kuheshimu cha mwenzio ni aina moja wapo ya kuomba kwa maulana akuwezeshe kupata kile walichonacho. Mungu ni mwerevu. Hawezi kukupa unachotamani wakati na umejaza chuki na ghiliba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *