AY: Joh Makini ni rapper mkali kuliko yeyote aliyetokea miaka 9 iliyopita

AY: Joh Makini ni rapper mkali kuliko yeyote aliyetokea miaka 9 iliyopita

2
242
0
Friday, 03 April 2015
habari

Joh Makini si wamchezo mchezo. Rapper AY amefunguka kuhusu uwezo wake kwenye muziki wa Hip Hop nchini.

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumatano hii, AY amedai kuwa hakuna rapper aliyemzidi Joh katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.

“Hakuna rapa mwingine aliyeingia kwenye ‘game’ baada ya mwaka 2008 akawa mkali kumzidi Joh Makini,” amesema AY.

Kwa sasa Joh ameachia nyimbo mpya ‘Waya’ huku AY na yeye akiwa ameachia wimbo mpya ‘More and More’ aliomshirikisha Nyashinski kutoka Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *