Baba yangu aliuawa – Paris Jackson

Baba yangu aliuawa – Paris Jackson

Like
175
0
Monday, 09 February 2015
habari

Mtoto wa Michael Jackson, Paris anaamini kuwa baba yake aliuawa.

MJ alifariki June 25, 2009. Akizungumza kwenye mahojiano na jarida la The Rolling Stone, Paris alisema, “Alikuwa akielezea kuhusu watu waliokuwa wakimtafuta. Kuna wakati alisema ‘watakuja kuniua siku moja.’ Msichana huyo anasema kila mmoja kwenye familia yake anaamini kuwa kulikuwa na mpango mchafu dhidi ya baba yake.

Anadai kuwa siku moja atapata haki yake. “Ni mchezo wa chess. Na ninajaribu kucheza mchezo wa chess vizuri.”

Amemnyooshea vidole pia daktari wake, Dr. Conrad Murray, aliyehukumiwa kwa kusababisha bila kukusudia kifo cha baba yake. Pia anawalaumu AEG Live, mapromota wa show za baba yake.

“AEG Live hawatendei haki wasanii wake. Huwachosha na kuwafanyisha kazi hadi wanakufa.” Paris ana wasiwasi pia Justin Bieber anayefanya kazi na kampuni hiyo kuwa yanaweza kumkuta ya baba yake.

Ameeleza kuwa mara nyingi baba yake alikuwa amechoka lakini alikuwa hawezi kupata usingizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *