Ben Pol, Christian Bella, G-Nako na Dogo Richie kuwasha moto Mombasa

Ben Pol, Christian Bella, G-Nako na Dogo Richie kuwasha moto Mombasa

Like
299
0
Thursday, 02 February 2017
habari

Wasanii wakali wa Bongo Flava, Ben Pol, Christian Bella na G-Nako pamoja na mkali wa kibao kinachotamba kwa sasa nchini Kenya, ‘Mziki Majanga’, Dogo Richie aka Richie Ree, usiku wa Jumamosi, Feb 25 wanatarajiwa kuporomosha burudani lukuki hapa mjini Mombasa.

Show hiyo iliyopewa jina la BONGO CONNECT inaandaliwa na kudhaminiwa na promoter maarufu wa muziki wa kizazi kipya Kenya, Baba Tee na mmiliki wa kampuni ya kupromote wanamuziki ya KingKong Entertainment.

MaMc wa show hiyo watakuwa watangazaji wa kituo cha redio cha Pilipili FM 99.5 Mombasa akiwemo Mc Gates Mgenge, Chriss Da Bass na Tucker The Entertainer.

Pia onesho hilo litanakishiwa na wanasanturi ama Djs watatu maarufu kutoka mjini Mombasa, akiwemo Dj Ivory, Dj Riley na Dj Smith. Show hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki mjini Mombasa, haswa ikitarajiwa kuwa show ya kwanza kubwa kufanyika ya kiaina yake, itakayowaleta mastaa watatu wa level za A kutoka Bongo, huku Christian Bella mkali wa masauti na nyimbo za dansi akitarajiwa kupigilia msumari kibao chake kipya ‘Ollah’ alichomshirikisha rapper makali wa hapa nchini Kenya, Khaligraph Jones.

Ben Pol ana umarufu uliopitiliza mjini Mombasa, hasa baada ya kutoa kibao Sophia ambacho wengi hapa uswahilini (Mombasa) mji wa kale wamekivulia kofia bila kusahau vibao kama Moyo Mashine, Ningefanyaje alicho mshirikisha Mrembo Avril, kisha kuwarusha mioyo na modern Afro pop kwa kibao ambacho kimemuinua level za juu mwanamuziki wa Bongo flava mwenzake, si mwingine ila rapper mkali kwa hivi sasa Darassa, hapa hatari tupu tu.

Staa G-Nako, anavyopeta Mombasani usipime, tangu enzi za Nako 2 Nako Soldiers, wakitoa vibao kama Ndio zetu, SweetSixsteen, Bado Ngware na vibao vingine.

Wakati huo huo, inakuwa fursa nyingine maridhawa kwa msanii Dogo Richie kutanua mabawa zaidi kwa ku-connect na mastaa hawa watatu kutoka Bongo kimuziki kupitia show hiyo. Tayari kuna tetesi kuwa msanii Rabbit aka Kaka Sungura, ameingia studio na Richie kufanya Refix ya ngoma ‘Mziki Majanga’ Na mashabiki kote nchini Kenya wamekuwa wakizidisha kutoa hisia mseto kuhusu nyimbo hiyo. Na hii huenda ikawa sababu kuu ya organisers wa show hii kumchagua staa huyo wa #MzikiMjanga kulikwea jukwaa moja na Ben Pol, G-Nako na Christian Bella.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *