Carlos Santana: Beyoncé ni model, sio muimbaji

Carlos Santana: Beyoncé ni model, sio muimbaji

Like
197
0
Wednesday, 15 February 2017
habari

Mpiga gitaa maarufu wa Marekani, Carlos Santana anaweza kuwa amewachokoza nyuki wa Beyonce.

Baada ya Adele kunyakua tuzo kubwa za Grammy ikiwemo Album of the Year aliyokuwa akishindana na Beyoncé, Santana amesema Queen Bey alikosa sababu sio muimbaji. “Nadhani Adele alishinda kwasababu anaweza kuimba,” aliimbia Australian Associated Press.

“Kwa heshima na taadhima kwa dada yangu Beyoncé, Beyoncé ni mzuri sana kumwangalia ni kama muziki wa ulimbwende, sio muimbaji,” aliongeza. “Adele anaweza kuimba. Haleti dancers wote, huweza kusimama tu pale na kuimba wimbo na hivyo tu, na ndio maana anashinda.”

Hata hivyo Jumapili Adele alidai kuwa album ya Beyonce, Lemonade ilipaswa kushinda tuzo ya album bora. “I can’t possibly accept this award,” alisema Adele wakati amepanda jukwaani kupokea tuzo.

“I’m very humbled, and very grateful, and very gracious, but the artist of my life is Beyoncé. This album to me, the LEMONADE album, was so monumental, Beyoncé. It was so monumental, well thought-out, beautiful, and soul baring, and we all got to see another side to you that you don’t always let us see and we appreciate that. All us artists here adore you. You are our light.”

Kuonesha kuwa alikuwa hatanii Adele aliigawanisha tuzo yake mara mbili ili kipande kimoja ampe Beyonce. Hadi sasa Beyoncé ameshinda Grammy 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *