Dayna Nyange atoa somo kwa wasanii wanaoandikiwa nyimbo zao

Dayna Nyange atoa somo kwa wasanii wanaoandikiwa nyimbo zao

Like
177
0
Wednesday, 01 February 2017
habari

Dayna Nyange ametoa somo kwa wasanii ambao hawana uwezo wa kuandika nyimbo zao.

Hitmaker huyo wa Komela, amekiambia kipindi cha E News cha EATV Jumanne hii, wasanii wajifunze kuandika kwani wanaweza wakapata bahati ya kufanya kazi na msanii mkubwa duniani wakaanza kuhangaika.

“Siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali kwa kuwa hujui kuandika,” amesema Dayna.

Dayna ameongeza kwa kumpongeza Maua Sama kutokana na uwezo wake wa kuandika nyimbo zake ambazo zimeonekana kumfurahisha zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *