Ilinichukua saa moja tu kurekodi cover ya ‘Upepo’ ya Recho – Ray C

Ilinichukua saa moja tu kurekodi cover ya ‘Upepo’ ya Recho – Ray C

1
466
0
Tuesday, 24 January 2017
habari

Kwa muda wote ambao Recho alikuwa akifanya muziki, sauti yake ilikuwa ikifananishwa na ile ya Rehema Chalamila aka Ray C. Na Upepo, ni moja kati ya nyimbo za Recho zilizowahi kufanya vizuri.

Sasa imagine, wimbo huo ukiimbwa na Ray C mwenyewe! Hatari. Muimbaji huyo mkongwe amepokea pongezi nyingi wiki hii kutokana na kufanya cover ya wimbo huo itakayojumuishwa kwenye album ya Valentine’s Day.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Loudspika cha Africa Swahili FM kinachoendeshwa na Ergon Elly kuwa ilimtumia saa moja tu kurekodi wimbo huo.

“Niliifanya siku nne zilizopita, tumeingia studio na Ima the Boy na tumetumia lisaa limoja tu,” amesema. “Ni nyimbo ambayo nilikuwa naisikiliza na naipenda kwahiyo nilikuwa nayo kichwani, huwa naisikiliza sana kwahiyo ilikuwa ni rahisi tu,” ameongeza.

Ray C amesema anapenda sana kazi za Recho na humchukulia kama mdogo wake anayempenda sana. Kwa upande mwingine Rehema amesema kazi zake mpya zitaanza kusikika mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *