Kitu P Funk amesema baada ya kumualika Harmorapa kumtembelea studio

Kitu P Funk amesema baada ya kumualika Harmorapa kumtembelea studio

1
214
0
Tuesday, 07 February 2017
habari

Harmorapa umaarufu wake umeanzia tu kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii akijifananisha na mwimbaji wa WCB Harmonize na baada ya hapo ndio akaanza ku-trend.

Leo February 6 2017 producer maarufu wa Bongo Records P Funk Majani ambaye anazo sifa nyingi za kuwa hodari wa kuwatoa Wasanii wengi, amemualika Harmorapa kwenye studio yake na kuipost picha wakiwa pamoja na ikazua maswali mengi.

AyoTV  imempata P Funk na akakubali kujibu maswali ya ilikuaje wakakutana na mpaka akamualika studio ambapo amejibu >>> “Amekuja kiushkaji tu alitaka kuja kuniona kupata ushauri kwahiyo nimemualika tu amefika fresh nimemuelekezamuelekeza

Nimesikiliza nyimbo zake nimemuweka sawa tu na kumwambia ukweli, anaonekana kama anaandika… uwezo wa kuandika anao lakini anachana zile za kizamani, sasa nikawa nampa mbinu za kisasa jinsi ya kudandia kwenye beat na kucheza nazo

Kila mtu ameanza sehemu flani, hata mimi siku za kwanza nilikua nagonga beat mbaya… ni kitu tu kukitaka na kukijenga moyoni utakipata…. kwasababu watu wote wanamtolea macho nimemwambia usifanye kitu cha kipuuzi, utapoteza mashabiki wote ukifanya kitu takataka

Ni mtu ambaye anaelewa sana na ana roho nzuri, ana heshima sana…. ni baraka za Mungu ndio maana naona watu wanampenda sana, ana heshima sana…. tumsaidie bwana !! kuhusu kurekodi nae studio kwangu hapana…. bado hajafika hapo nimemwambia kabisa kuna siku itafika lakini sio sasa hivi… mpaka ukajirekebishe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *