Kumbe ni kweli ‘One Dance’ ya Drake imeandikwa na Wizkid!

Kumbe ni kweli ‘One Dance’ ya Drake imeandikwa na Wizkid!

Like
185
0
Tuesday, 07 February 2017
habari

Kumbe ni kweli Wizkid ndio aliyemuandikia Drake wimbo wa ‘One Dance’! Wimbo huo umefanikiwa kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali mpaka Billboard.

ASCAP wamethibitisha hilo kutokana na kadi hiyo hapo chini ambayo imeonekana kusambaa mitandaoni.

Naye Wizkid hakushindwa kuonyesha furaha yake baada ya mchango wake kuonekana katika wimbo huo, kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika, “This came in last night! Big up my bro @champagnepapi for letting me work on this!! More Drake x Wizkid on the way!! 😈.”

Mwezi Juni mwaka jana Seyi Shay alimwaga mchele kwenye kipindi cha On Stage wakati alipokuwa nchini Jamaica kwa kufunguka kuwa Wizkid ndio ameuandika wimbo huo kwa kushirikiana na baadhi ya watu wa nchini Nigeria. Kitendo hicho kilimfanya Wizkid amjie juu Seyi lakini baadaye waliyamaliza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *