Ngoma yangu ijayo nimemshirikisha Muisrael – Azma Mponda

Ngoma yangu ijayo nimemshirikisha Muisrael – Azma Mponda

1
212
0
Wednesday, 25 January 2017
habari

Baada ya kufanya vizuri na ngoma yake ya Astara Vaste aliyompa shavu Belle 9, rapper Azma Mponda ameweka wazi mipango yake ya kuvuka boda za +255 ili kujitangaza zaidi.

Rapper huyo ambaye anajivunia kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube kupitia ngoma yake ya ‘Jinsi ya Kumfikisha Mpenzi’, ameiambia Super Mega ya Kings Fm kuwa project yake ijayo ataifanya nje ya nchi.

“Baada ya Astara Vaste, kuna project kubwa sana inakuja, kwa taarifa tu, ni project ambayo nimefanya na mzungu mmoja kutoka Israel ambaye anaishi Kenya, ni balozi wa Israel Kenya anaitwa Gillad,” amesema Azma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *