Ninafanya mpango wa kumshirikisha Davido, pia kukutana na Justin Bieber

Ninafanya mpango wa kumshirikisha Davido, pia kukutana na Justin Bieber

Like
190
0
Friday, 03 February 2017
habari

Malaika hakwenda Marekani kushangaa maghorofa, bali kutafuta kila connection inayoweza kumpaisha juu kimuziki.

Akizungumza na DJ Haazu wa Radio5 ya Arusha, hitmaker huyo wa Zogo, amedai kuwa tayari ameshafanya collabo na msanii mkubwa wa Sierra Leone. Kama hiyo haitoshi, Davido na Justin Bieber nao wapo kwenye menu.

“Mpaka sasa hivi nimefanya kazi na msanii mkubwa kutoka Sierra Leone na pia amenilink-up pamoja na Davido so nafikiri tutafanya kazi,” amesema Malaika.

 

“Na sasa hivi tunafanya kazi ya kukutana na Justin Bieber pia, sababu nimepewa ndani ya siku 10 ndio nitaweza kumuona, yupo kwenye ratiba zake zingine,” ameongeza muimbaji huyo.

Kuhusu kama amepanga kumshirikisha Bieber, Malaika amesema, “Oh Yeah, sasa hivi ndio ipo inafanyiwa kazi soon nafikiri itakavyokuwa tayari watatuona tukiwa studio. Lakini pia naweza kusema kuwa nimefanya kazi na producer ambaye ametengeneza ngoma ya Beyonce, Drunk in Love, kwahiyo kazi ipo tayari, na tunasubiria mixing, itakapokuwa tayari tutaitoa.”

Pamoja na kwamba Bieber ni miongoni mwa mastaa vipenzi vya watoto wa kike, Malaika amedai kuwa akipata nafasi hiyo hatokuwa na wazo lolote zaidi ya kazi.

“Actually nilivyosikia kwamba anaweza kupatikana Bieber mimi kufanya naye kazi na akawa ametoa hizo siku 10, mawazo yangu hayakuwa kuanzisha mahusiano, mawazo yangu yalikuwa kazi, kwahiyo nategemea kazi sana kwa Bieber kuliko vitu vingine.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *