Nuh Mziwanda ataja majina mawili aliyopanga kumuita mwanae, akiwa wa kike atakuwa na jina kama la mtoto wa Mwana FA

Nuh Mziwanda ataja majina mawili aliyopanga kumuita mwanae, akiwa wa kike atakuwa na jina kama la mtoto wa Mwana FA

Like
301
0
Wednesday, 08 February 2017
habari

Mshawasha wa baba na mama kupata mtoto huwa na hisia za aina yake. Na kwa mwanaume anayetarajia kupata mtoto toka kwa mkewe anayempenda kwa dhati, hamu yake huwa haielekezeki.

Wakati ambapo Nuh Mziwanda na mkewe wanasubiria ujio wa mtoto wao wa kwanza, muimbaji huyo ameshachagua majina mawili ya kumpa mtoto wao akizaliwa. Akiwa wa kiume watamuita Travis na akiwa wa kike watamuita Malikah – Mtoto wa kike wa Mwana FA naye anaitwa jina hilo japo huandikwa tofauti, Maleeka.

“Mama Travis or Malikah if God wishes,” ameandika Mziwanda kwenye Instagram. Na kama unajiuliza kwanini hadi sasa Nuh hajui mtoto huyo atakuwa na jinsia gani wakati teknolojia imewezesha watu kujua mapema, yeye ameamua kwenda ‘the oldschool way’, anapenda surprises!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *