muziki

Ray Vanny kuja na ngoma aliyomshirikisha Diamond Ray Vanny kuja na ngoma aliyomshirikisha Diamond
habari

Good News kwenye muziki wa Bongo Fleva wiki iliyopita ni Ishu ya watanzania Diamond Platnumz,Alikiba na Navy Kenzo kushinda tuzo za Hipipo Music Awards huko Uganda. Moja ya tuzo alizoshinda Diamond ni tuzo ya Video bora East Africa kupitia video ya Salome aliyomshirikisha msanii wa label yake, Ray Vanny. Baada ya ushindi huo, Raymond amefunguka kuhusu kufanya tena ngoma a Diamond ambapo amedai kuwa itakuwa ni ngoma yake yeye. “Lazima,watu wasubiri,” amesema Ray kupitia Supermega ya Kings Fm. Tayari Rich...

Like
275
0
Tuesday, 07 February 2017
Kumbe ni kweli ‘One Dance’ ya Drake imeandikwa na Wizkid!
habari

Kumbe ni kweli Wizkid ndio aliyemuandikia Drake wimbo wa ‘One Dance’! Wimbo huo umefanikiwa kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali mpaka Billboard. ASCAP wamethibitisha hilo kutokana na kadi hiyo hapo chini ambayo imeonekana kusambaa mitandaoni. Naye Wizkid hakushindwa kuonyesha furaha yake baada ya mchango wake kuonekana katika wimbo huo, kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika, “This came in last night! Big up my bro @champagnepapi for letting me work on this!! More Drake x Wizkid on the way!! 😈.” Mwezi Juni...

Like
200
0
Tuesday, 07 February 2017
Ben Pol, Christian Bella, G-Nako na Dogo Richie kuwasha moto Mombasa
habari

Wasanii wakali wa Bongo Flava, Ben Pol, Christian Bella na G-Nako pamoja na mkali wa kibao kinachotamba kwa sasa nchini Kenya, ‘Mziki Majanga’, Dogo Richie aka Richie Ree, usiku wa Jumamosi, Feb 25 wanatarajiwa kuporomosha burudani lukuki hapa mjini Mombasa. Show hiyo iliyopewa jina la BONGO CONNECT inaandaliwa na kudhaminiwa na promoter maarufu wa muziki wa kizazi kipya Kenya, Baba Tee na mmiliki wa kampuni ya kupromote wanamuziki ya KingKong Entertainment. MaMc wa show hiyo watakuwa watangazaji wa kituo cha...

Like
299
0
Thursday, 02 February 2017
Nicki Minaj na Drake wapiga picha ya pamoja baada ya kupita miaka miwili
habari

Ni muda mrefu Nicki Minaj na Drake hawajaonekana katika picha ya pamoja. Ni takribani miaka miwili wawili hawa hawajaonekana pamoja huku ikichangiwa na bifu la Drake na ex wa zamani wa Nicki, Meek Mill. Jumatano hii wawili hao wameonekana katika picha ya pamoja wakiwa na rapper Lil Wayne. “#TheBIG3 #YoungMoney 🎀 ~ 📸,” ameandika Minaj katika moja ya picha alizoaiweka katika mtandao wa...

Like
262
0
Thursday, 02 February 2017
Trace TV leo kuanza kuionesha video ya ‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo
habari

Baada ya takriban miaka miwili tangu urekodiwe, hatimaye wimbo wa Diamond aliomshirikisha msanii wa Marekani, Ne-Yo, ‘Marry You’ unatoka rasmi, Jumatano hii. Ni Trace TV ndiyo inakuwa ya kwanza kuionesha video hiyo. Kituo hicho cha runinga kimepost video ya staa huyo kwenye Twitter akielezea kuhusu kurushwa kwa video yake. Tayari Youtube wimbo huu umewekwa kwenye utitiri wa channel lakini ulikuwa haujawahi kuachiwa rasmi. Video ya wimbo huo ilifanyika Marekani mwaka jana. Awali, video ilikuwa itoke mapema zaidi, lakini ratiba ilibadilika...

Like
194
0
Wednesday, 01 February 2017
Kanye West ataja tarehe ya kuachia Yeezy Season 5
habari

Baada ya kupata matatizo ya ugonjwa na kukaa kimya kwa muda mrefu, Kanye West anajipanga kuachia nguo zake za Yeezy Season 5, Februari 15 mwaka huu. Onesho hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Pier 59 Studios uliopo jijini New York. Awali fashion show yake ya Yeezy Season 4 iliangukia pua kitendo ambacho kilimfanya rapper huyo kufukuza wafanyakazi wake wote 30 na kuamua kujikita katika ziara yake ya Saint...

Like
141
0
Wednesday, 01 February 2017
Mimi nafanya kazi kama kichaa – Vanessa Mdee
habari

Msanii wa muziki Vanessa Mdee amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mmoja kati ya wanawake ambao wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maisha yake yanaenda sawa. Akiongea katika kipindi cha Wanawake Live cha EATV wiki hii, Vanessa amedai yeye ni mwanawake ambaye wanafanya kazi kwa bidii huku akidai tayari amejipangia ratiba ya kazi zake mpaka mwezi wa nne. “Mimi nafanya kazi kama kichaa, kwa sababu kuna vitu ambavyo najua natakiwa nivitimize kwa muda fulani. Kwa hiyo najua nikivitimiza, nitakuwa...

Like
161
0
Wednesday, 01 February 2017
Selena Gomez na The Weeknd hakuna siri tena
habari

Mapenzi ni kama kikohozi kikikushika huwezi kuficha. Mapenzi ya Selena Gomez na The Weeknd sasa hayana siri tena. Wawili hao wameonekana wakiwa katika hoteli ya kifahari ya Belmond Villa San Michele iliyopo mjini Venice, Italia ambapo wameweka kambi kwa ajili ya mapumziko yao wakitokea Florence. Imedaiwa kuwa kulala usiku mmoja katika hoteli hiyo inagharimu kiasi cha dola 4,000 hadi 7,000. Hoteli hiyo ni maarufu zaidi kwa kufikiwa na mastaa mbalimbali duniani ambapo hata Kanye West na mkewe Kim Kardashian waliwahi...

Like
172
0
Wednesday, 01 February 2017
Makampuni yamiminika kudhamini 40 ya mtoto wa Diamond
habari

Watoto wa Diamond Platnumz huzaliwa wakiwa na harufu za ustaa unaotoka kwa baba na mama yao, Zari The Bosslady. Wakati Tiffah akiendelea kushikilia taji la mtoto staa kuliko wote Afrika, mdogo wake Nillan yuko nyuma kufuata nyayo zake. Makampuni takriban matano yamejitokeza kudhamini sherehe za Nillan kutimiza siku 40, ambapo kwa mara ya kwanza sura yake itaoneshwa. Sherehe hizo zitafanyika wiki moja...

Like
166
0
Wednesday, 01 February 2017
Dayna Nyange atoa somo kwa wasanii wanaoandikiwa nyimbo zao
habari

Dayna Nyange ametoa somo kwa wasanii ambao hawana uwezo wa kuandika nyimbo zao. Hitmaker huyo wa Komela, amekiambia kipindi cha E News cha EATV Jumanne hii, wasanii wajifunze kuandika kwani wanaweza wakapata bahati ya kufanya kazi na msanii mkubwa duniani wakaanza kuhangaika. “Siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali...

Like
176
0
Wednesday, 01 February 2017