Tunaweza kupata album ya Mwana FA iwapo mipango hii ikienda sawa

Tunaweza kupata album ya Mwana FA iwapo mipango hii ikienda sawa

1
183
0
Monday, 30 January 2017
habari

Nani asiyependa kumiliki album mpya ya mmoja wa waandishi wakali wa mashairi ya hip hop wa muda wote kutoka Tanzania – Hamis ‘Mwana FA’ Mwinjuma? Kama wewe ni mmoja wa mashabiki damu damu na Binamu, basi tuombe Mungu mipango iliyopo mezani mwake ifanikiwe ili tupatiwe fursa hiyo adimu kwenye muziki wa leo.

“Tuna muziki mwingi ndani, kama kutotolewa kwa album kutaendelea, inawezekana kuna nyimbo hazitokaa zisikike maisha yote,” FA ameiambia Bongo5.

FA amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakitafuta utaratibu ambao wanaweza kuanza kutoa album tena lakini kila anayehusika ikamlipa.

“Kwahiyo utaratibu kama tunataka kuufanya hivi,” anasema. “Kuna mwekezaji mmoja ametokea hivi anataka kama kuinvest kwenye haya masuala. Bado tunajadiliana naye, sisemi kwamba tumekubaliana tutatoa album, lakini tupo kwenye mazungumzo na yanakwenda vizuri. Pengine siku chache hizi kama atakuwa ameturudia, tutajua kama album inaweza kutoka mwaka huu. Album kwasababu ipo tayari ni vichache tu vimesalia, namna ya kuziunganisha nyimbo, sehemu ambapo zinakutana, theme ya album, covers na vitu vidogo vidogo,”ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *